Licha ya urafiki mkubwa walionao, Wanandoa Jay Z na Beyonce waipotezea harusi ya mshkaji wao Kanye West

gauni1
Hatimaye Rapa maarufu wa muziki wa nchini Marekani Kanye West na mwanadada anayemake headlines kila kukicha Kim Kardashian wamefunga pingu za maisha na kuwa mume na mke huko Florence nchini Italia. Wapenzi hao walisafiri kwa nyakati tofauti kutoka jijini Paris nchini Ufaransa ambako waliungana na familia zao katika ile Pre Wedding Party.....>>>>

Taarifa zinadai kuwa wanandoa hao wapya walipanga kufunga ndoa hiyo huko Chateau de Versailles lakini sheria za Ufaransa hazikuwaruhusu kufanya hivyo kutokana na hata mmoja wao kutokuwa na uraia wa nchi hiyo.
Cha kushangaza ni kwamba si Jay Z wala Mke wake Beyonce aliyehudhuria katika harusi hiyo na kuishia kutuma salamu za pongezi licha ya kuwepo kwa uvumi kuwa Jay Z atakuwa msimamizi wake kutokana na ukaribu na urafiki mkubwa waliokuwa nao.
Tukio hilo kubwa limehudhuriwa na wageni mbalimbali na watu mashuhuri akiwemo mwanamuziki John Legend na mkewe Chrissy Teigen na muongozaji wa filamu ya 12 Years a Slave Steve McQueen.
Story nyingine kubwa ni kwamba mabosi wa kampuni ya Adidas pia walichagua siku hiyo ya harusi kuzindua tangazo lao la kombe la dunia kwa mwaka 2014 linalomhusisha rapa Kanye West pamoja na mastaa wakubwa wa soka duniani Lionel Messi na Dani Alves.
harusi1harusi2harusi3harusi5
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks