Hayati Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu wa 21

SONY DSCRipota wa nguvu Albert G. Sengo kutoka Mwanza anaripoti Mmisionari Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza ujumbe kuhusu hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu wa 21 tangu tarehe 20/03/2013...>>>>

SONY DSCPicha ya mwisho ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere aliyopiga kijijini kwake Butiama kabla ya kwenda kupata matibabu nchini Uingereza ambapo alifia katika Hospitali ya Mt. Thomas.
Wakati yote haya yakifanyika kutoka nchini Uganda: Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki.
Rais Museveni aliyasema hayo Tarehe moja mwezi June, wakati wa ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu.
SONY DSCPicha ya mchoro wa Mtakatifu Charles Lwanga aliyemtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa Mtakatifu wa 21 ambapo alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye.
Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba Mwalimu Nyerere ana sifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu.
simon4Mmisionari Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza ujumbe kuhusu Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu wa 21 akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliotembelea kaburi la Baba wa Taifa Butiama mkoani Mara.
Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwa unganisha Waafrika.
Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka kubwa.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks