Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Kapteni John Komba likiwa limebebwa kuelekea kwenye jukwaa maalum kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Familia ya Marehemu Kapteni John Komba ikiwa imesimama tayari kuupokea mwili wa marehemu kwenye viwanja vya Karimjee
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa pamoja na Makamu wa Rais Ghalib Bilal (kushoto) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Marehemu Kapteni John Komba uliagwa na Viongozi mbali mbali na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais Ghalib Bilal kwenye viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Kapteni John Komba ulikuwa unaagwa
Viongozi wa CCM pamoja na wanamuziki wa muziki wa dansi wakiimba kwa pamoja nyimbo maalum wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
Mzee Yusuf Makamba akifuta machozi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni CCM Dk. Mohamed Seif Khatib akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
Kada wa CCM na Mwanasiasa mkongwe nchi Kingunge Ngombale Mwilu akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
Waziri wa Mambo ya Nje na uhusiano wa Kimataifa Bernad Membe akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
0 comments:
Post a Comment