![]() |
Waamuzi
wakijadiliana jambo NBA
|
1564: Shakespeare azaliwa
WILLIAM Shakespeare alikuwa
mtunzi wa mashairi na mwigizaji raia wa Uingereza ambaye anachukuliwa kama
ndiye mwandishi mkubwa wa lugha ya kiingereza. Alizaliwa Stratford-upon-Avon.
Alipofikisha miaka 18 alimuoa Anne Hathaway ambaye walizaa watoto watatu,
Susana na mapacha Hamnnet na Judith.
Kati ya mwaka 1585-1592 alikuwa maarufu kwa uigizaji jijini London. Alifariki
Aprili 23, 1616.
1988: Waamuzi watatu waanza kutumika NBA
CHAMA cha Mpira wa
Kikapu nchini Marekani (NBA) kilipitisha
matumizi ya waamuzi watatu katika mechi
mbalimbali za Ligi Kuu nchini humo.
Kanuni hiyo ilianza kutumika kwa mara ya kwanza msimu wa 1988-89 tangu
kuanzishwa kwa ligi hiyo Juni 6, 1946 jijini New York.
2014: Lee Marshall afariki dunia
MARSHALL Aaron Mayer alikuwa
mtangazaji wa mieleka nchini Marekani chini ya Mwavuli wa Chama cha Mieleka
nchini humo (AWA), pia World Championship Wrestling (WCW) na Women Wrestling
(WOW).
Alizaliwa Novemba 28,
1949 Los Angeles alikuwa akijulikana kwa jina ‘Stagger Lee’ akijiunga na timu
ya watangazaji wa mchezo huo wakati wa mapambano mbalimbali katika runinga ya
ESPN.
Atakumbukwa kwa sauti
yake iliyokuwa na mvuto yenye kuamsha shangwe ukumbini wakati wa mchezo huo akiwapandisha
jukwaani wakali mbalimbali. Alifariki Santa Monica, California.
0 comments:
Post a Comment