Kinara wa kuuza madawa ya kulevya mbaloni


Kinara wa wauzaji madawa ya kulevya Mexico akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Kinara wa wauzaji madawa ya kulevya Mexico akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Kiongozi wa genge kubwa la wauza madawa ya kulevya Servando Gomez alikamatwa katika oparesheni iliyotekelezwa katika jimbo la Michoacan nchini Mexico hapo jana.
Kiongozi huyu wa kundi lililowahangaisha wananchi wa Mexico alikuwa mlengwa wa kwanza wa jitihada za Rais Enrique Pena Nieto za kupambana na wauzaji wa madawa ya kulevya nchini humo.
Serikali ilikuwa imeahidi zawadi ya dola milioni 2 kwa mtu ambaye angesaidia kukamatwa kwa kiongozi huyo.
Kabla ya kujiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya Servando Gomez alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.
Gomez atafikishwa mahakamani kujibu jumla ya mashtaka 8 yanayomkabili.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks