Glavu za ngumi zilizovaliwa na Muhammad Ali na Sony Liston kwenye pambano lao la marudiano maarufu la uzito wa juu mwaka 1965 zimezoa pauni 622,000 (bil. 1.7) kufuatia mnada uliofanyika New York siku ya Jumamosi.
Kampuni ya mnada ya Herritage Auctions yenye maskani yake mjini Dallas, ambao walishikilia mauzo hayo, walisema glavu hizo zilinunuliwa na mnunuzi ambaye hakutaka kufahamika.
Pambano hilo ambalo alishinda Muhammad Ali kwenye raundi ya kwanza kwa kumuangusha chini Sonny Liston lilifanyika katika mji wa Lewiston Maine Mei 25 1965, na hivi karibuni litatimiza miaka 50, litakumbukwa daima kama “ngumi nene” (phanton punch).
0 comments:
Post a Comment