Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Israel ametaka Waarabu wote
wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wakatwe
vichwa.Avigdor Lieberman alisema hivyo jana kuwa, inabidi vichwa vya Waarabu wote wanaoishi katika ardhi za Palestina kwa mabavu vitenganishwe na miili yao.
Waziri huyo mwenye misimamo mikali amesema: “… kila anayetupinga hapaswi kupewa fursa yoyote ya kuishi lazima tuchukue shoka na kuwakata vichwa vyao vinginevyo hatutaweza kukaa salama hapa.” Mwanasiasa huyo kutoka chama chenye misimamo mikali cha Yisrael Beytenu amesema hayo katika kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi huu.
Mara kwa mara Lieberman amekuwa akitoa maneno yaliyojaa chuki dhidi ya Waarabu akiwaita kuwa wote ni magaidi na kutaka kutolewa hukumu za kifo kwa kila Mwarabu anayepinga siasa za Israel.
Amewahi pia kuutaka utawala wa Israel uwashambulie kwa mabomu ya nyuklia Waislamu wa Palestina wanaishi katika Ukanda wa Ghaza.
0 comments:
Post a Comment