![]() |
Patrick Mafisango mwaka 2012
|
1972: Tottenham yatwaa Kombe la UEFA
KOMBE la Ligi ya Europa linavyojulikana kwa sasa lilianza mwaka 1971, na timu ya kwanza kulitwaa ilikuwa Tottenham Hotspur jijini London ilipoibanjua Woverhampton Wanderers kwa uwiano wa mabao 3-2.
1989: Napoli yatwaa taji la Europa
SSC Napoli ni miongoni mwa klabu 27 zilizotwaa taji la Ligi ya Europa ikifanya hivyo katika michuano ya 18 mjini Stuttgart ikimzabua VFB Stuttgart kwa uwiano wa mabao 5-4 huku timu za Uingereza zikikosekana kwa msimu wa nne. Nyota wa klabu hiyo Diego Maradona alikuwa mchezaji wa kutegemea kwa asilimia zote.
2012: Mafisango afariki dunia
PATRICK Mafisango akijulikana kwa jina la Papaa au Petit alikuwa mchezaji wa Simba SC na raia wa Rwanda aliyezaliwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Alifariki kwa ajali jijini Dar es Salaam katika eneo la Keko ikiwa ni siku chache baada ya klabu ya Simba kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara. Akiitumikia klabu hiyo katika nafasi ya kiungo alifunga mabao 13. Alizikwa jijini Kinshasa Mei 22, 2012. Alizaliwa Machi 9, 1980.
2014: Arsenal yatwaa Kombe la FA
WASHIKA Bunduki wa Kaskazini mwa London, Arsenal walitwaa taji la FA ikiitandika Hull City kwa mabao 3-2 katika uga wa Wembley. Hii ilikuwa FA ya kwanza kufanyika mwisho mwa msimu wa Ligi Kuu. Aaron ramsey aling’ara sana katika mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment