Filamu ya maisha ya Nuhu na gharika 'Noah' yapigwa marufuku nchi za kiarabu.

Filamu ya maisha ya Nuhu na gharika

Filamu hiyo imepigwa marufuku kwa madai kuwa kwanza inazua mtazamo tofauti kutokana na utofauti uliopo kati ya Biblia na Quran kuhusu simulizi la Nuhu na gharika ingawa kuna mfanano katika vitabu hivyo vitakatifu kuwa kulitokea mafuriko na Mungu akamwambia Nuhu ajenge safina.
Sababu ya pili ni kuonesha mfanano wa nabii na muigizaji wa kawaida hali inayoweza kuzua hisia tofauti kwa baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu.
Mkurugenzi wa maudhui ya vyombo vya habari wa umoja wa nchi/falme za Kiarabu (National Media Centre-United Arab Emirates), Juma Al-Leem, ameiambia Associated Press kuwa filamu hiyo haitaruhusiwa kwenye nchi hizo kwa kuwa inakinzana na miiko katika dini ya kiislam hasa katika kumfananisha nabii na mtu wa kawaida.
“Kuna vipande vya filamu hiyo ambavyo vinakanganya (simulizi) kati ya Biblia na Uislam, kwa hiyo tumeamua kuacha kuionesha.” Alisema Juma Al-Leem. “Ni muhimu kuheshimu dini hizi mbili na kuacha kuonesha filamu hiyo.
Taasisi ya kiislamu ya Al-Azhar ya Misri, imeeleza kuwa imeikataa filamu hiyo kwa kuwa iko kinyume na mafundisho ya dini hiyo na kwamba kuonekana kwa kukataa kuonesha taswira ya mtu ikifananishwa na ile ya nabii kutasaidia kuepuka watu kuanza kumuabudu mtu badala ya Mungu.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks