hii imetokea korea baada ya wanandugu kuunganishwa tena leo, waliopotezana takribani miaka 60 iliyopita!!!!!!


Makundi kadhaa ya watu wakongwe kutoka Korea Kusini wanaelekea Kaskazini kukutana na jamaa zao ambao hawajaonana kwa zaidi ya miaka sitini, tangu vita vilivyotenganisha mataifa hayo mawili ya rasi ya Korea.>>>>>>>>


Wakongwe hao wamebeba mikoba iliyojaa zawadi, ikiwa ni pamoja na dawa za maradhi ya kawaida, picha za familia na vyakula.
Tukio hilo litakaloibua majonzi litafanyika katika eneo la kitalii upande wa Korea Kaskazini.
Hapajakuwa na zoezi kama hilo la kuunganisha familia tangu mwaka 2010.
Awali Korea Kaskazini imefutilia mbali mpango huo wa kuziunganisha familia kujibu vitendo vya Korea Kusini ambavyo Kaskazini inapinga.
Shirika la Msalaba Mwekundu linasema kuwa watu alfu sabini wanaoishi Kusini wanasubiri fursa ya kukutana na jamaa zao wa Kaskazini-nusu kati ya watu hao ni wazee walio na umri wa zaidi ya miaka 80.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks