Kama hukuwahi kubahatika kutembelea Singapore basi Marina Bay ni moja kati ya sehemu ambazo unapaswa kutembelea kama utafanikiwa kufika Singapore. Marina Bay ni uwanja wa mpira wa miguu ambao unaelea kwenye maji, yaani sehemu ya kuchezea inaelea ila majukwaa yapo nchi kavu.
Marina Bay umejengwa
kwa vyuma lakini unaelea na unatajwa kuwa na uzito wa tani 1,070 ambazo
ni sawa na uzito wa watu 9000, upande wa jukwaa la mashabiki lina uwezo
wa kubeba watu 30,000. Uwanja huo toka mwaka 2007 umekuwa ukitumika kwa
shughuli mbalimbali kama soka, michezo mingine, matamasha, maonyesho ya
sanaa pamoja na sherehe za kitaifa zinazohusisha gwaride la askari
jeshi na polisi.
0 comments:
Post a Comment