Hii ni Taarifa kutoka Mahakamani kuhusu kesi ya msanii AT na Mganga wa jadi.
Ukiniuliza kuhusu stori ambazo zimesomwa sana kwenye internet mwaka huu nchini Tanzania, hii ya msanii AT na mganga wake nayo imo kwenye orodha.
Hii story ilianzia kwenye You Heard ya February 06 2014 ambapo ilimuhusu mtu anaesemekana kuwa Mganga wa AT aliyekuwa akilalamika AT kakimbia na deni lake.
Leo March 10 2014 kesi ya Mganga huyu wa jadi Dr. Sharrif imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya mwanzo Buguruni Dar es salaam ambapo AT amesomewa mashitaka yake ambayo aliyakanusha yote.
Kesi imehairishwa mpaka tarehe 04 April 2014 ambapo mdai ambae ni huyu Mganga ametakiwa kwenda na vielelezo vyote ili kuthibitisha madai yake.
Kwenye maelezo ya Mganga Sharrif, amedai kati ya mwaka 2010 na mwaka 2013 alimpatia matibabu AT na hakumlipa pesa yake ya matibabu hayo ambayo yalikuwa ni ya kuinua nyota yake na kumpatia tuzo za kili ya mwaka 2013 na mengineyo.
0 comments:
Post a Comment