Mwanasiasa mmoja mwakilishi wa Wodi, nchini Kenya ameshitakiwa kwa madai ya kumtusi Rais Uhuru Kenyatta katika mkutano wa kisiasa uliofanyika katika jimbo la Kisii Magharibi mwa Kenya
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, mwakilishi huyo wa wodi ya Kiogoro Samuel Aboko Onkwani, anadaiwa kusema maneno haya:
''Washirika wa karibu wa Rais Uhuru Kenyatta wanapaswa kumshauri awache kuvuta Bhangi.’’
Bwana Onkwani alifikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la kuhujumu mamlaka ya afisa wa umma...>>>>>
Anadaiwa kutoa matamshi hayo mwezi Agosti mwaka 2013, katika jimbo la Kisii Magharibi mwa Kenya.
Mahakama iliambiwa kuwa matamshi ya Aboko yalidhamiria kumharibia sifa Rais Kenyatta ambaye ni afisaa wa Umma.
Bwana Aboko alikanusha madai hayo.
Mawakili wake waliomba mahakama kumwachilia kwa dhamana na pia waweze kukabidhiwa kanda iliyorekodiwa kuonyesha kuwa kweli Bwana Boko alitoa matamshi hayo.
Pia wameomba upande wa mashitaka kuwakabidhi taarifa ya mashahidi katika kesi hiyo.
Hata hivyo upande wa mashitaka umesema kuwa haiwezekani upande wa utetezi kupata ushahidi wanaotaka kwani afisa aliyechunguza kesi hiyo hakutoa ushahidi huo kwa mahakama.
Mahakama ilimwachilia Aboko kwa dhamana ya dola 589. Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 14 mwezi Mei.
0 comments:
Post a Comment