Gwiji wa Man U auponda mfumo wa Louis van Gaal


Gwiji wa Manchester United Paul Scholes ameuponda mfumo wa Louis van Gaal wa kutumia 3-5-2 kwenye klabu msimu huu, kwa mujibu wa makala yake kwenye gazeti la Independent.
Nyota huyo wa zamani wa Uingereza anaguswa na ulinzi wa timu yake ya zamani, ambayo ilifungwa 4-0 na timu ya League One ya MK Dons mapema wiki hii...>>>>

United hawajashinda tangu msimu wa Ligi Kuu uanze, wakianza kwa kufungwa na Swansea City, Old Trafford, na kutoa suluhu 1-1 dhidi ya Sunderland kwenye mechi ya pili.
“Watu watatu nyuma hawawezi kufanya kazi kwake mpaka sasa,” alisema Scholes.
“Kwa sasa United wanaonekana kuruhusu magoli mara kwa mara.”
“Naelewa Van Gaal anajaribu kufanya mabadiliko haraka ila tatizo ni wachezaji wanaonekana kushindwa kuendana na mfumo wa 3-5-2 mpaka sasa.”
“Sio rahisi kufanya mabadiliko ya kiufundi kwa kipindi kifupi kwa wachezaji waliozoea kucheza na wakiwa na watu wanne nyuma kwa miaka mingi.”
Mchezaji huyo, 39, pia anahisi kwamba viungo watano na winga sio njia nzuri ya kumtumia Angel Di Maria ili wanufaike naye.
“Sidhani Di Maria atakwenda kucheza kama winga katika mfumo wa 3-5-2. Naweza kumuona akicheza pembeni katika mfumo wa 4-4-2 au 4-4-1-1,” aliongeza.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks