nchini marekani kikundi cha familia kinatarajiwa kupeleka mashtaka mahakamani dhidi ya vyama sita vya mpira wa miguu ,pamoja na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA,kwa lengo la kutaka uboreshwaji wa sheria za usalama michezoni...>>>
Mashtaka hayo ambayo yamefunguliwa katika mahakama moja mjini California,yanadai kua Fifa haijafanya lolote kuzuia ajali za kichwani pindi wachezaji wawapo michezoni.katika kile walicho pendekeza kama sheria mpya,watoto walio chini ya umri wa miaka 17, wanapaswa kuupiga mpira kwa kutumia kichwa mara kadhaa kwa hesabu maalumu ambayo inapaswa kuwekwa na mchezaji asizidishe kiwango.
Lakini pia watoe ruhusa ya muda mbadala ya kuwafanyia uchunguzi wachezaji kama wamepata madhara kichwani.
0 comments:
Post a Comment