Leo katika historia Ijumaa, Februari 27, 2015

Ivan Petrovich Pavlov
Leo ni Ijumaa tarehe 8 Mfunguo Nane Jamadil Awwal 1436 Hijria,  sawa na Februari 27, 2015 Milaadia.
Miaka 79 iliyopita katika siku kama hii ya leo mwaka 1936 alifariki dunia Ivan Petrovich Pavlov, tabibu na mtaalamu mkubwa wa elimu ya biolojia wa Russia akiwa na umri wa miaka 87. Alizaliwa mwaka 1849 katika familia ya kidini na mwaka 1879 alihitimu elimu ya udaktari. Tabibu huyo alikuwa na shauku kubwa ya kufanya utafiti kuhusu miili ya wanyama inavyofanya kazi. Mbali na kufanya utafiti mkubwa kuhusu mzungumo wa damu, Pavlov alifanikiwa kugundua nadharia ya 'conditional reflex' katika wanyama, suala ambalo lilimfanya utunukiwe Tuzo ya Nobel mwaka 1904.
Siku kama ya leo miaka 73 iliyopita sawa na tarehe 27 Fabruari 1942 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, yalianza mashambulizi makubwa ya ndege za Japan dhidi ya vituo vya majini vya nchi waitifaki. Mashambulizi hayo yalitokea katika Bahari ya Java. Idadi kubwa ya meli za kivita za Marekani, Australia na Uingereza zilikuwa zimejizatiti katika bahari hiyo ambayo ipo katika maji ya Bahari ya Pasifiki. Mapigano hayo makubwa yalimalizika kwa kuzama idadi kubwa ya meli za nchi hizo tatu na kupata ushindi manowari za kijeshi za Japan.
Na siku kama ya leo miaka 4 iliyopita alifariki dunia Waziri Mkuu wa zamani wa Uturuki Najmuddin Erbakan akiwa na umri wa miaka 84. Baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Istanbul, Erbakan alijiunga na Chuo Kikuu cha Aachen nchini Ujerumani ambako alipata shahada ya uzamivu. Mwaka 1969 Najmuddin Erbakan aliingia katika uwanja wa siasa na kuchaguliwa katika Bunge la Uturuki. Mwaka 1987 aliongoza chama chenye mielekeo ya Kiislamu cha Refah ambacho kilipata viti vingi vya bunge na kumteuwa kuwa Waziri Mkuu mwaka 1996. Tukio hilo liliwakasirisha mno wanasiasa wa kilaiki wa Uturuki, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Serikali ya Erbakan ilipigwa vita na jeshi la Uturuki na miezi 10 baadaye chama cha Refah kilivunjwa na wanajeshi, na mwanasiasa huyo akapigwa marufuku kujishughulisha na masuala ya kisiasa kwa kipindi cha miaka 5.
Pf. Najmuddin Erbakan anatambuliwa kuwa baba wa harakati ya Kiislamu ya Uturuki
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks