Tiger Woods aporomoka vibaya
Tiger Woods ameporomoka kwenye orodha ya wacheza gofu 100 kwa mara ya kwanza katika mchezo huo.
Mshindi mara 14, ambaye mara ya kwanza kuingia katika 100 bora ilikuwa 1996 na kuendeleza rekodi hiyo kwa wiki 683 kama nambari moja duniani, ameporomoka hadi nafasi ya 104.
Mmarekani huyo 39, hajacheza tangu ajitoe kwenye Farmers Insurance Open Februari 6.
Woods alisema ana matumaini ya kurudi na kuwa juu mwaka huu, kwenye Masters, akianzia Aprili 9.

0 comments:
Post a Comment