Kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal, Bayern ilikuwa haijapoteza hata mchezo mmoja kati ya michezo 12 iliyokuwa imecheza msimu huu kwenye mashindano yote huku ikiwa imefunga jumla ya magoli 40.
Olivier Giroud alianza kuifungia Arsenal goli la kwanza dakika ya 77 ikiwa ni dakika tatu tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Theo Walcott aliyepumzishwa kumpisha nyota huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa.
Giroud alifunga goli hilo akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Santi Cazorla.
Mesut Ozil iliihakikishia Arsenal pointi tatu baada ya kufunga goli la pili dakika ya 90 ya mchezo huo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Hector Bellerin.
Mchezo huo unakuwa ni wa kwanza kupoteza msimu huu kwa upande wa The Bavarians wakati ushindi huo kwa Arsenal ni wa kwanza kwenye michuano hiyo kwenye msimu huu.
Licha ya kutawala mchezo mchezo huo kwa asilimia nyingi, bado haikutosha kwa wakali hao wa Bundesliga kutoka Ujerumani kuchukua pointi tatu mbele ya Arsenal.
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kukusanya paointi tatu za kwanza kwenye michuano hiyo na kujikita nafasi ya tatu huku Bayern wakiwa kileleni mwa kundi F kwa kuwa na pointi sita sawa na Olympiacos lakini wakitofautiana wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Arsenal ina pointi sawa na Dinamo Zagreb (pointi tatu) lakini The Gunners wanakaa juu kwa wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa jana usiku ni kama ifuatavyo:
0 comments:
Post a Comment