Dodoma yafurika, wajumbe wawasili vyumba vyaadimika


  • Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, jumla ya hoteli 27 zimeainishwa kuwapokea wajumbe hao 640 ambao wanatarajiwa kuwapo mjini Dodoma kwa muda wa miezi mitatu.

Dodoma.Wakati Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwasili mjini Dodoma, Ofisi ya Bunge imetangaza kuandaa utaratibu wa malazi kwa wajumbe hao katika hoteli mbalimbali mjini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, jumla ya hoteli 27 zimeainishwa kuwapokea wajumbe hao 640 ambao wanatarajiwa kuwapo mjini Dodoma kwa muda wa miezi mitatu.
Pamoja na utaratibu wa malazi, taarifa hiyo pia iliagiza wajumbe hao kuwasili wakiwa na nakala halisi za vitambulisho vitakavyotumika kwa ajili ya usajili.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa usajili utafanyika leo na kesho kwenye Ofisi za Bunge, ambapo zoezi hilo litajumuisha ujazaji wa fomu, upigaji picha za vitambulisho sambamba na kukabidhiwa vitendea kazi.
Baada ya zoezi hilo Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi watakutana na wajumbe kwa ajili ya kutoa maelekezo ya awali yanayohusiana na utaratibu wa ukaaji, jiografia ya viwanja vya Bunge na huduma za utawala.
Kikao cha kwanza cha mkutano huo kitafanyika Jumanne ijayo, ambapo pamoja na masuala mengine kitahusisha uchaguzi wa mwenyekiti wa muda atakayesimamia upitishwaji wa kanuni na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge hilo.
Wiki iliyopita Ikulu ilitangaza majina ya wajumbe 201, yaliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushiriki katika uchambuzi wa Rasimu ya Pili ya Katiba na kutengeneza Katiba Mpya.
Mbali ya wajumbe wa Bunge la Katiba, pia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wako Dodoma wakiendelea na vikao vyao.
Mji wafurika wageni
Kutokana na kuwapo kwa ugeni huo, Mji wa Dodoma umefurika wageni wakiwamo wajumbe wa Bunge la Katiba na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) huku, maeneo mengi yakionekana kufanyiwa usafi.
Hata hivyo, wageni wengi walionekana kuingia jana na baadhi ya watumishi wa hoteli hizo walikiri kuwasajili baadhi ya wageni, ambao wapo katika orodha hiyo.
Gazeti hili jana lilishuhudia kukiwa na maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mapokezi hayo, huku baadhi ya maeneo yakiendelea kukarabatiwa ikiwamo kupaka rangi.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks