hii ni Kuhusu Daktari feki aliyekamatwa Muhimbili leo.















Leo February 25 Uongozi wa hospitali ya taifa muhimbili kwa kushirikiana na maafisa wake wa usalama wamemnasa daktari feki aliyekuwa akiwatapeli fedha wagonjwa na watu mbalimbali wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
Taarifa kutoka Muhimbili inasema ni Tukio la tatu kutokea katika hospitali hiyo ingawa matukio ya namna hiyo yameshawahi kuripotiwa katika baadhi ya hospitali kubwa za serikali kwa baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa fani ya udaktari kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Msemaji wa Hospital ya taifa Muhimbili Aminieli Aligaesha amemtaja Daktari huyo feki kwa jina la Kitano Mustapha na kubainisha kuwa katika upekuzi uliofanywa na maofisa usalama wa hospitali hiyo wamemkuta mtuhumiwa akiwa na kadi tatu za kliniki,namba za simu za madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria zilizopo na kanuni za utabibu.
Daktari huyo feki Kitano Mustapha amekana kutohusika na utaperi huo kwa wagonjwa mbali mbali wanaofika kupata huduma za kimatibabu na kusema hawezi kuongea lolote mpaka Mwanasheria wake awepo.
powered by millardayo
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks