Picha 7 za mwigizaji Lulu Mahakamani leo na maelezo yake. {powered by millardayo}

'loggo1Leo February 17 kutoka Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam mwigizaji Elizabeth Michael maarufu Lulu alikuwa akisomewa shitaka lake la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Steven Kanumba April 07 2012 Vatican Sinza Dar es salaam.
Akisoma maelezo ya awali wakili wa serikali Monica Mbogo mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba, amesema siku ya tukio kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mshtakiwa na baadaye mshtakiwa aliondoka usiku wa saa sita baada ya marehemu kuanguka chumbani ambapo alfajiri ya february 07  saa 11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo la Bamaga.


2
Wakili Peter Kibatala ambaye anamtetea Lulu amesema wameridhishwa na sehemu kubwa ya  maelezo ya awali ya mteja wao ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa tena huku kila upande ukitarajia kuleta mashahidi watatu.
Wakili Kibatala ameongea na millardayo.com na kusema >>> ‘leo kulikua na hatua mbili za kisheria huku ya kwanza ikiwa ni Mshtakiwa kusomewa shitaka na anasema kama anakiri au anakataa ambapo leo mshitakiwa amekataa shitaka, hatua nyingine ni kukubaliana kwa pande mbili za Utetezi na mashtaka kuhusu maeneo gani ya kishahidi na kisheria ambayo tunakubaliana nayo na yale tusiyokubaliana, huu ni utaratibu wa kisheria kuhakikisha kesi zinachukua muda mfupi’
‘Hayo ndio tuliyofanya leo ambapo kesi itaendelea kwa ratiba za Kimahakama, sisi kazi yetu kwa sasa ni kulinda maslahi ya mteja wetu Lulu… leo kisheria ni ile siku ya mshtakiwa kusomewa kosa ambapo sisi tumelikataa na baada ya hapo tukafanya maelezo ya awali ili baada ya hapo Mahakama iweze kupanga ratiba ya kesi kutokana na vitu gani tunabishania na tusivyobishania’

1
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria leo mahakamani kumsindikiza Lulu ni pamoja na Dr.Cheni na Kajala.

4
Lulu ambae muda wote alionekana kwenye hali ya utulivu Mahakamani hakutakiwa kujibu chochote leo

6
7

loggo2
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks