Pistorius-Kesi yake kwendelea kuzua utata sasa kupeperushwa moja kwa moja hewanu


Jaji mmoja nchini Afrika Kusini ameamua kuwa sehemu za kesi dhidi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius zinaweza kupeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni.
Pistorius anadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mchumba wake Reeva Steenkamp, zaidi ya mwaka mmoja uliopita, na kesi dhidi yake itaanza kusikilizwa Jumatatu ijayo
.
Wendesha wakuu wa mashitaka wanadai kuwa mauaji hayo yalipangwa ingawa mwenyewe anadai kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi ndani ya nyumba yake.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa kesi nchini Afrika Kusini kupeperushwa moja kwa moja hewani kupitia televisheni.
Jaji Dunstan Mlambo alitakiwa kueleza muda ambao kesi hiyo itapeperushwa moja kwa moja. Ombi hilo lilitolewa na mashirika ya habari ya MultiChoice, eNCA na Eyewitness News.
Sauti pia zitanaswa na kupeperushwa hewani huku wapiga picha wakiruhusiwa kunasa picha
Hata hivyo mawakili wa mtuhumiwa wanasema kuwa ikiwa hilo litaruhisiwa itaweza kuathiri kesi kwa njia moja au nyingine kutokana na hukumu za watu dhidi ya mshukiwa.
Marehemu Steenkamp, aliyekuwa na umri wa miaka 29, alipigwa risasi mara tatu kupitia kwa mlango wa choo, nyumbani kwa Pistorius mjini Pretoria masaa ya asubuhi mwaka jana wakati wa siku ya Valentine.
Pistorius hata hivyo alijitetea aliposema kuwa alidhani kwamba mwizi alikuwa amevamia nyumba yake ndio maana akaamua kumpiga risasi asijue kama ni mpenzi wake na pia amekanusha madai ya upande wa mashitaka kuwa yeye na mpenzi wake waligombana kabla ya tukio la mauaji.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks