Tuzo Za Kili 2014 Zimezinduliwa Leo, Fahamu Alichosema George Kavishe Na Mabadiliko ya tuzo hizo Hapa.
Tuzo za kili zimeanza rasmi mwaka 1999 na mambo mengi yameboresha baada ya wadau wa muziki Tanzania kutoa sababu zao.
Kili Music awards 2014 mwaka 2014 zimezinduliwa tarehe 17/2/2014. Brand Manager wa Kilimanjaro Bei amesema haya kuhusu mwaka huu.
1] mwaka huu Watanzania watapigakura kwa njia ya simu {sms] kuchagua msanii gani aingie kwenye category gani. Itakuwa kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia February 18 2014 category zote zitaonyeshwa na kura zitapigwa kwenda 15440, Unachagua msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye category gani.
2] Kura zitapigwa mara 2, ya kuingia kwenye kipengele na yakushinda tuzo.
3] Timu ya watu 100 ikiwa na Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki watafatilia tu kuhusu wimbo kuwa kwenye mwaka husika,pia kipengele sawa na kama unavigezo vya kuingia kwenye tuzo hizi.
Note, Mabadiliko ya Tuzo za mwaka Huu Ndio Haya.
1] 2014 KTMA itakua na vipengele 36 na category 34 ni za kupigiwa kura na mbili ni zile category maalum za kuteuliwa tu. Mwaka jana palikuwa na vipengele 37, Imetolewa ya - Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka Huu.
2] Vipengele vimebadilishwa majina Ndio Hivi
- Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana.
- Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume
-Mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
-Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya Msanii bora wa kiume bongofleva.
-Mwimbaji bora kiume band Badala ya msanii bora wa kiume band.
-Mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya msanii bora wa kike bongofleva.
-Mwimbaji bora wa kike Taarab badala msanii bora wa kike Taarab.
-Mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.
-Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia.
-Video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo ya mwaka.
-Wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongo pop.
-Wimbo bora wa vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili tu.
Note Sababu Ya Mabadiliko Ya Mwimbaji na sio Msanii.
-Neno Msanii linapendekeza maana zaidi ya moja. Mfano Msanii wa sanaa ya Uchoraji Na Hata Uigizaji.
Mabadiliko Ya Vipengele Yapo Chini Ya Basata.
safi
ReplyDelete