Inawezekana kabisa mbegu ya mapenzi aliyoipanda Nelly kwenye moyo wa mkali wa RnB Ashanti bado inaendelea kukua ingawa waliachana miaka kadhaa iliyopita.
Katika party ya uzinduzi wa albam yake ‘Braveheart’, Ashanti alionekana akiongea na mtu kwa njia ya simu huku akimwagia mabusu kadhaa. Baada ya muda aliionesha ‘screen’ ya simu yake hadharani ili kumuonesha kila mtu na ikaonekana picha ya Nelly..>>
Hii ilimaanisha kuwa alikuwa anaongea na Nelly na kumfanyia yote hayo huku akitabasamu muda wote.
Bado haijajulikana moja kwa moja kama wawili hao wamerudiana tayari ama ni hatua za kutaka kurudiana.
0 comments:
Post a Comment