GUINEA: Uuzaji na usambazaji wa nyama ya POPO wazuiwa ili kuzuia kuenea kwa EBOLA



Popo hutumiwa kutengeza kitoweo maarufu sana katika baadhi ya maeneo ya Guinea, lakini sasa inahofiwa kuwa popo wanachangia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kusini mwa nchi hiyo.
Maafisa nchini humo sasa wamepiga marufuku uuzaji na ulaji wa nyama ya popo katika juhudi za kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola, ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62...>>>

Nchi za kanda hiyo zikiwemo Liberia na Sierra Leone, zimechukua hatua kabambe kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa kiafya watu wanaongia mipakani.
Maafisa wa afya wanapata msaada kutoka shirika la afya duniani na ujumbe wa kuhamasisha watu unapeperushwa kupitia televisheni.
Watu watano kati ya sita walioingia nchini Liberia kutoka Guinea walikua na ishara za ugonjwa huo na wamethibitishwa kufa.
Hatahivyo maafisa wa utawala nchini Liberia bado hawajathibitisha kikamilifu kama kweli walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks