Madereva wa malori wamegoma kuendelea na safari baada ya mwenzao kuvamiwa.


  Madereva wa malori zaidi ya mia tatu wamegoma kuendelea na safari katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao aliyekuwa akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki manispaa ya Singida.
Wakiongea na chanzo chetu madereva ambao wamekutwa katika eneo hilo wameomba  jeshi la polisi kufanya doria mara kwa mara eneo hilo kwani kumekuwa na matuki  yanayo jirudia ya utekeji wa magari  kwa kuweka mawe makubwa barabarani na kuwajeruhi madereva jambo ambalo lina tishia amani kwa watumiaji wa barabara.

Madereva wa malori baada ya kufunga barabara naibu waziri wa Afrika mashariki Dr. Abdulla Abdulla alikumbwa na adha hiyo na kusema ni haki ya kikatiba kwa madereva kugoma kwa kudai haki zao, kutokana na hali hiyo amewahaidi madereva kupeleka kilio chao katika mamlaka husika ili kuweza kutatua tatizo lao na kukomesha vitendo vya uvamizi wa magari katika eneo hilo .
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida  SACP Geofrey Kamwela amesema madereva waliamua kusimama barabarani bila sababu yeyote kwa muda wa zaidi ya masaa matatu na kusababisha foleni kubwa ambapo kwamujibu wa sheria za usalama barabarani walikuwa wamefanya kosa ,lakini baada ya viongozi kufika na kuwasikiliza waliamua kuendelea na safari.
Naye dereva wa lori bwana Agustino Mbawala aliye tekwa, akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiongea kwa shida huku akiwa na maumivu makali amesema aliona mawe makubwa barabarani na kuamua kusimama na kukimbia lakini wali mvamia na kumpiga hatimaye  kumpora fedha na simu. 
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks