Zaidi ya watu 70 wameuawa katika milipuko miwili ambayo imetokea katika kituo cha mabasi mjini Abuja, Nigeria.


Zaidi ya watu 70 wameuawa katika milipuko miwili ambayo imetokea katika kituo cha mabasi mjini Abuja, Nigeria.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja, Haruna Tangaza anasema milipuko hiyo ilitokea wakati abiria wakiwa katika harakati za kupanda mabasi na teksi wakienda maofisini katikati ya mji wa Abuja.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema miili ya watu imetapakaa katika eneo la tukio.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Boko Haram ambalo limehusishwa na mashambulio ya awali nchini humo pia limehusishwa na milipuko hiyo...>>>

Hata hivyo, mashambulio mengi ya kundi hilo yamekuwa yakifanyika kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Abbas Idris, mkuu wa Shirika la Misaada la Nigeria, ameiambia BBC kwamba wamethibitisha watu 71 kuuawa na wengine 124 kujeruhiwa.
Msemaji wa polisi Frank Mba ametoa takwimu kama hizo, akiongeza kuwa mabasi 16 ya kifahari na mabasi madogo 24 yameharibiwa.
Mmoja wa walioshuhudia mlipuko huo, Badamsi Nyanya ameiambia BBC kuwa ameona miili 40 ikiondolewa. Watu wengine walioshuhudia tukio hilo wanasema wamewaona wafanyakazi wa uokoaji na polisi wakiokota sehemu za miili zilizotawanywa na milipuko hiyo.
Mlipuko huo ulichimba chini mita 1.2 katika viwanja vya Nyanya Motor Park, kiasi cha kilomita 16 kutoka katikati ya jiji, na kuharibu zaidi ya magari 30, na kusababisha mlipuko zaidi kutokana na matangi ya mafuta ya magari hayo kushika moto na kuwaka.
Magari ya wagonjwa yamekuwa yakibeba miili ya watu waliokufa na wale waliojeruhiwa katika hospitali za karibu.
Shuhuda mwingine Bi Mimi Daniels, ambaye anafanya kazi mjini Abuja, anasema: "nilikuwa nasubiri basi niliposikia mlipuko mkubwa halafu nikaona moshi," ameiambia Reuters.
"Watu walikuwa wakikimbia ovyo kutokana na taharuki."
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks