APPLE YANUNUA HEADPHONE ZA DR DRE KWA DOLA BILIONI 3




dre-e1399586836803Kampuni kubwa ya teknolojia Apple imethibitisha kwamba itanunua vipokea sauti na huduma ya kusikiliza muziki kupitia kwenye mtandao wa inteneti kutoka kampuni ya Beats Electronics katika makubaliano ya dola bilioni 3.
Hayo yakiwa ni makubaliano makubwa katika historia ya miaka 38 ya kampuni hiyo......>>>>>>
Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza muziki kwenye mtandao.
Pamoja na ununuzi huo, waanzilishi wa Beats Jimmy Lovine na msanii wa mziki mtindo wa kufoka Dkt. Dre watajiunga na kampuni hiyo ya kiteknolojia
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook alisema kuwa mkataba huo ungewezesha kampuni hiyo ‘kuendelea kutengeneza bidhaa na huduma za muziki zenye ubunifu duniani.’

Beats ilianzishwa na mzalishaji wa muziki Jimmy Lovine na nyota wa mziki wa kufokafoka, Dr. Dre, na mitambo hiyo imejulikana kuwa bora zaidi hadi siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple ina huduma ya iTunes ambayo ndio kubwa zaidi duniani inayohusiana na mziki, na ilianzisha kituo cha radio cha iTunes mwaka uliopita.
Hata hivyo, huduma ya mziki ya Beats ina wateja wapatao 110,000 pekee waliojisajili ikilinganishwa na Spotify ilio na watu milioni 10 waliojisajiliwa.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks