Kuhusu Pacha waliozaliwa Wakiwa wakishikana mikono Marekani

Mama wa mapcha hawa amesema mapacha wake ni zawadi kubwa kwake
Mama mmoja nchini Marekani, amejifungua watoto pacha wakiwa wameshikana mikono.
Watoto hao pia walikuwa wanapumua bila usaidizi wowote walipotolewa kutoka katika mashine yenye hewa ya Oxygen....>>>>

Mama wa watoto hao, alisema kuwa watoto hao waliopewa majina ya Jillian na Jenna Thistlewaite walikuwa wameshikana katika kitovu na kutumia Kondo moja la nyuma , hali ambayo madaktari walisema ni nadra.
"Tayari wanaonekana kuwa marafiki ,’’ alisema mama yao Sarah Thistlethwaite.
Walizaliwa Ijumaa katika jimbo la Ohio, wakiwa wameshikana mikono.
Inaarifiwa ni mama mmoja tu kati ya akina mama elfu kumi mwenye uwezo wa kujifungua watoto pacha wa aina hiyo.
Bi Thistlewaite, mwenye umri wa miaka 32,alilazimika kupumzika kwa wiki kadhaa kabla ya kujifungua kwani pacha wanaozaliwa wakiwa wameshikana mikoni ni hali nadra ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watoto na mama kabla ya kuzaliwa.

Mama huyo alisema kupokea watoto wake ilikuwa zawadi tosha kwake wakati huu wa kusherehekea siku ya akina mama duniani.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks