Polisi wanamchunguza David Moyes, anadaiwa kumpiga huyu kijana kwenye hii baa

Screen Shot 2014-05-23 at 8.12.31 AMKocha David Moyes ambae alifukuzwa kuiongoza Manchester United mwezi uliopita alikwenda kwenye hii Baa yeye na rafiki zake ambapo kwenye mida ya saa nne usiku ishu ndio ikatokea.
Polisi wa Lancashire ndio wanachunguza kuhusiana na madai ya shambulio lililotokea Wine Bar baada ya kudaiwa yeye na wenzake kuhusika kumchambulia kijana wa miaka 23 kwenye baa hiyo huko Clitheroe usiku wa Jumatano...>>>>>>

Screen Shot 2014-05-23 at 8.10.02 AMHata hivyo kijana alieshambuliwa hakuhitaji matibabu yeyote hivyo hakwenda hospitali lakini hilo halijalishi manake
Polisi wanaendelea kupitia rekodi za video za camera za CCTV za eneo hilo ili kujua kila kilichotokea na aliehusika.
“Kulikua na mashambulizi nje ya bar hii lakini hakuna mfanyakazi aliyeumia, polisi wanashughulika na uchunguzi mpaka sasa”Alisema mzungumzaji wa Bar hiyo.
Screen Shot 2014-05-23 at 8.12.16 AMPamoja na kwamba Polisi hawajatoa ripoti, mmoja wa mashuhuda amesema huyu kijana alipigwa na Moyes baada ya kumtusi. kumchana kuhusu kufukuzwa kwake Man United na kumwita jina la kitu ambacho hakijawahi kufanikiwa au kupata ushindi.
Huu ugomvi ulitokea nje tu ya baa hiyo kwenye meza na viti ambapo kwenye purukushani glasi zilitupwa chini na kijana huyu kuumia kichwani na begani baada ya yeye na kundi lake kuanza kutoa vijembe walipomuona David Moyes.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks