Sakata la Kampuni ya Samsung na Wafanyakazi wake

                 


Kampuni kubwa duniani ya vifaa vye elektroniki, Samsung inasema kuwa itawalipa fidia wafanyakazi wake waliougua Saratani kutokana na kufanya kazi katika viwanda vyake.
Kampuni hiyo iliomba radhi kwa kesi ya muda mrefu kati yake na wafanyakazi hao waliokuwa wanadai fidia na badala yake kukubali kujiondoa katika kesi hiyo huku ikikubali kuwalipa fidia wagonjwa hao.
Hatua ya Samsung kukubali kuwalipa wafanyakazi hao inaleta matumaini katika kukamilika kwa mvutano huo ambao ulionekana kukwama kwa muda mrefu...>>>>

Lakini afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Kwon Oh-hyun nusura kukiri kuwa kulikuwa sababu ya wafanyakazi hao kupatwa na Saratni ilichangiwa na wao kufanya kazi katika kiwanda cha Samsung. Wengi walipata Saratani ya damu au Leukaemia.
Bwana Kwon alisema wafanyakazi kadhaa katika viwanda vyetu walipatwa na Saratani ya damu na kuugua magonjwa mengine yasiyokuwa na tiba ambayo yalisababisha baadhi yao kufariki.''
"tulipaswa kumaliza kesi hii kitambo sana na bila shaka tunahisi uchungu kwamba tulikosa kufanya hivyo, tunaomba radhi kwa hilo. ''
Akiongea na wandishi wa habari, Bwana Kwon alisema kuwa Samsung inatumai kuwa itaweza kumaliza kesi hii na kuweza pia kuwapa afueni wagonjwa na familia zao.''
Hata hivyo kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya simu za Smartphone haikusema idadi ya watu watakaolipwa fidia ingawa inaarifiwa ni watu 40 waliowasilisha malalamiko hayo huku kesi ikiendelea kwa zaidi ya miaka sita.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks