TETESI ZA USAJIRI NA TAARIFA MBALIMBALI ZA SOKA KATIKA MAGAZETI YA ULAYA.

TETESI ZA SOKA WEEKEND HII
Meneja Wa Arsenal Arsene Wenger yuko tayari kutumia kitita cha paundi milioni 100 za usajili baada ya yeye mwenyewe kusaini mkataba wa miaka mitatu (Daily Mail), QPR wanataka kumsajili beki wa Man City Joleon Lescott (Daily Mirror), klabu ya Montpellier ya Ufaransa imeiambia Newcastle lazima watoe paundi milioni 12 kumsajili kiungo mshambuliaji Remy Cabella (Guardian), rais wa Barcelona Josep...>>>
Maria Bartomeu amezionya Arsenal na Manchester United kuwa Cesc Fabregas hauzwi (Metro), Valencia watapambana vikali na Liverpool na Everton kusaka saini ya Thorgan Hazard, mdogo wake Edin Hazard wa Chelsea (Daily Express), Manchester United huenda wakawazidi kete Liverpool katika kumsaini kiungo wa Ukraine Yevhen Konoplyanka kutoka FC Dnipro (Talksport), Demba Ba anafanya mazungumzo na Besitkas kuhamia klabu hiyo ya Uturuki kwa paundi milioni 8 (Daily Mirror), Meneja mpya wa Barcelona Luis Enrique anataka Sergio Aguero wa Manchester City kuwa mchezaji wake wa kwanza kumsajili. Barcelona iko tayari kutoka Euro milioni 38 (Sport), mshambuliaji wa PSG Edison Cavani hatosikiliza dau la Man United kwa sababu United hawachezi Champions League msimu ujao, na atasalia Ufaransa (L'Equipe), Liverpool inajiandaa kutoa paundi milioni 20 kumnunua Alexis Sanchez kutoka Barcelona.
NA HATIMAYE...Takriban watu 700 katika jimbo la Catalan la Spain wamewapa jina la Messi, mbwa na paka wao. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, ni watu 10 tu wamewapa wanyama wao jina la Ronaldo wa Real Madrid. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks