Wamiliki wa Instagram wako serious kwa kile walichokisema. Sheria ya kutopost picha za utupu au mwanamke kuonesha maziwa haiangalii status wala umri...>>>>>
Mwanamke mmoja mwenye watoto wanne ameshitushwa na tukio la kufungiwa akaunti yake ghafla baada ya kupost picha ya mwanae wa kike mwenye umri wa miezi 19 tu akionesha kifua chake.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Courtney Adamo wa London, ambaye pia ni blogger alikuwa na followers 40,000 kwenye akaunti yake kabla hajafungiwa.
Amewalalamikia sana Instagram laini ameeleza kuwa baadaya kuwasiliana na wazazi wenzake akaambiwa kuwa sheria ya Instagram inaeleza kuwa ni marufuku kuweka picha ya mtoto anaetembea, akiwa kifua wazi.
Hata hivyo sheria hiyo inazidi kumchanganya mama huyo kwa kuwa anadai siku zote amekuwa akiona matangazo ya bidhaa za watoto wakiwa wamevaa nepi tu bila nguo yoyote.
0 comments:
Post a Comment