Kuhusu Miraa Kupigwa Marufuku UK yaanza kutekelezwa

Ni kilio nchini Kenya wakulima wakohofia kupoteza ajira
Marufuku ya utafunaji wa miraa nchni Uingereza inaanza kutekelezwa leo, nchini Uingereza. Mmea huo hutafunwa na watu wengi wenye asili ya kisomali , Yemen na Ethiopia,>>>>>>


Serikali ya Uingereza inasema kuwa kuharamishwa kwa Miraa nchini Uingereza inaambatana na hatua zilizochukuliwa na mataifa mengine ya Ulaya pamoja na Marekani ambako Miraa ni haramu.
Watumiaji wa mmea huo wanasisitiza kuwa sio hatari kuutumia na kwamba kuupiga marufuku ni ubaguzi dhidi ya jamii ambazo ni za wachache.
Mmoja wa watu ambao wamekuwa wakiutumia mmea huo, Aden Haj anasema alitelekezwa na familia yake ambayo haingeweza kustahamili utumiaji wake wa Miraa na anawataka watu kufahamu athari za kutumia Miraa.
Nchini Kenya ambako mmea huo unakuzwa, maelfu ya wakulima katika eneo la Meru sasa wanakabiliwa na tishio la kupoteza mamilioni ya pesa baada ya marufuku ya kusafirisha miraa nchini Uingereza kuanza kutekelezwa.
Hatua hiyo inajiri baada ya Uingereza kuharamisha utafunaji wa miraa nchini humo baada ya mmea huo kuorodheshwa miongoni mwa madawa ya kulevya.
Uingereza ni mojawepo wa mataifa ya bara Ulaya yaliyokuwa yakitoa soko kubwa zaidi kwa zao la miraa kutoka Kenya kutokana na idadi kubwa ya watu wa jamii ya wasomali wanaoishi nchini humo.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks