Nikisema INDIAN JONE'S au AIR FORCE ONE, Utakuwa Unamfaham Mwigizaji Harrison Ford, Fahamu Kilichompata

Harrison Ford
Mcheza filamu mkongwe wa nchini Marekani Harrison Ford anapatiwa matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyopata wakati akirekodi filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Star Wars...>>>>

Harrison Ford mwenye umri wa miaka 71 amevunjika kifundo chake cha mguu baada ya mlango wa eneo la kutengeneza magari kumuangukia wakati wakirekodi filamu katika studio za Pinewood nchini Marekani.
HarrisonFordHanSolo
Mwigizaji huyo wa Hollywood ambaye ameigiza katika filamu ya Star Wars ambapo sasa anarekodi sehemu ya saba ya mwendelezo wa filamu hiyo alikimbizwa hospitalini ambapo msemaji wa kampuni ya kutengeneza filamu amesema wataendelea kurekodi kama kawaida.
Filamu hiyo inaigizwa na wasanii wenginge wakubwa kama Lupita Nyong’o, John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar Isaac, Andy Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow.
Tukio hilo limetokea wakati wa mwendelezo wa sehemu ya saba ya war Stars ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks