Taarifa mpya kuhusu Luis Suarez, hii ndio adhabu atakayopata akikutwa na hatia ya kumn’gata mchezaji mwenzake.

luisss
Mchezaji wa Uruguay Luis Suarez atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa muda mrefu kucheza mechi zikiwemo za Kombe la dunia ikiwa atakutwa na hatia ya kumng’ata mchezaji mwenzake wa Italia Giorgio Chiellini....>>>

Shirikisho la soka duniani limeanzisha uchunguzi dhidi ya mchezaji huyo  baada ya kuonekana akimng’ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao ya kombe la dunia.
luis2
Chiellini amedai Suarez amemng’ata katika bega lake la kushoto lakini Suarez amejitetea kuwa mchezaji huyo alijigonga kwake.
Refari wa mechi hiyo hakuchukua hatua yoyote dhidi ya Suarez.
Ikiwa atapatikana na hatia, Suarez huenda akazuiwa kucheza mechi 24 au kwa miaka miwili.
Suarez mwenyewe tayari amejitetea katika vyombo vya habari nchini Uruguay.
Suarez anasema Kuna mambo fulani ambayo hutokea uwanjani na hadhani ni vyema kuanza kuzua kashfa kutokana na mambo kama hayo.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks