TETESI ZA SOKA ULAYA


TETESI ZA SOKA ULAYA
Manchester City wanakaribia kumsajili Fernando kutoka Porto kwa pauni milioni 15 (Daily Mirror), kiungo wa Arsenal Santi Cazorla amemtaka Mspanish mwenzake Cesc Fabregas kurejea Emirates (Metro), Edin Hazard amepewa jezi namba 10 msimu ujao. PSG wanamtaka kwa pauni milioni 61, lakini mwenyewe amesema hatoondoka baada ya kupewa namba 10 (Daily Mail), Diego Costa yuko karibu..>>
sana kusaini Chelsea kwa pauni milioni 32, kilichosalia tu ni vipimo vya afya (Telegraph), Louis van Gaal anaamini Uholanzi haina budi kumshukuru David Moyes kwa kumfanya Robin van Persie kuwa hatari zaidi katika Kombe la Dunia (Daily Mirror), Cesc Fabregas amekubali kusaini mkataba na Chelsea. Kilichosalia ni makubaliano ya ada ya uhamisho, Barcelona wakiwa wanataka Euro milioni 36 (Mundo Deportivo), Koke, Fabregas na Paul Pogba wa Juventus, wote wapo kwenye 'rada' za Chelsea ili kuchukua nafasi ya Frank Lampard (Evening Standard). Share tetesi hizi na wapenzi wote wa soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks