TTETESI ZA SOKA ULAYA
*Chelsea kumpora Khedira kutoka Arsenal
*Real wamtaka Welbeck
*Di Maria kwenda United
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
ataruhusiwa kutumia fedha zote, pauni
milioni 75 za mauzo ya Luis Suarez
kuimarisha kikosi chake (The Times), Meneja
wa Arsenal, Arsene Wenger anayetafuta
kiungo mkabaji anapanga kuwachukua Sami
Khedira, 27, na Lars Bender, 25 (Daily
Telegraph), hata hivyo Chelsea wapo tayari
"kuuteka" mchakato wa Sami Khedira na
kumsajili mchezaji huyo wa Real Madrid
(Daily Mirror), Crystal Palace wanakaribia
kumsajili Fraizer Campbell kutoka Cardiff
City (Guardian), Newcastle wanakaribia
kumsajili Emmanuel Riviere, 24, kutoka
Monaco, mchezaji huyo amehusishwa pia na
kwenda Arsenal, Stoke City na West Brom
(Evening Chronicle) Arsenal na Tottenham
wanamwania Loic Remy, 27, ingawa
Newcastle huenda wakafanikiwa kumsajili
mchezaji huyo wa QPR aliyecheza msimu
uliopita kwa mkopo (Talksport), Stoke wako
karibu kumsajili Bojan Krkic, 23, kutoka
Barcelona (Daily Star), Inter Milan
wanafikiria kumsajili beki kutoka Chile Gary
Medel, 26 anayechezea Cardiff (Sky Sports),
Manchester United na Chelsea
wanamgombea kiungo Alex Song, 26, na
Barcelona wako tayari kupokea pauni milioni
20 (Daily Star), Newcastle wamekubaliana
na Montpellier kumsajili kiungo
mshambuliaji Remy Cabella, 24 (Daily
Express), West Ham wamepata upinzani
kutoka Sevilla na AC Milan kumsajili
mshambuliaji wa Ecuador Enner Valencia
anayechezea Pachuca ya Mexico (Times),
Chelsea wanafikiria kutoa dau la pauni
milioni 7 kumchukua kiungo Adrien Rabiot,
19, kutoka Paris St-Germain (Daily Express),
Real Madrid wanafikiria kumchukua
mshambuliaji wa Manchester United Danny
Welbeck kuziba nafasi ya Alvaro Morata
anayetarajia kujiunga na Juventus (Daily
Star), Arsenal tayari wametangaza dau la
euro milioni 25 kwa Sami Khedira, ingawa
Chelsea nao wanamtaka kiungo huyo wa
Real Madrid (Daily Express), winga wa Real
Madrid Angel Di Maria amefikia
makubaliano ya maslahi binafsi na
Manchester United ya pauni 150,000 kwa
wiki, ingawa klabu hizo mbili
hazijakubaliana bado kuhusu ada ya
uhamisho. Di Maria anasakwa pia na PSG
na Monaco (Metro), mshambuliaji wa
Manchester United, Bebe, 23, anataka
kuhamia Benfica kwa uhamisho wa kudumu.
Bebe alikuwa kwa mkopo Pacos Ferreira ya
Ureno (A Bola), Arsenal wanakaribia
kumsajili beki wa kulia Javi Manquillo kwa
mkopo kutoka Atlètico Madrid (Daily
Telegraph), Tottenham wanajiandaa kutoa
dau la pauni milioni 18 kumsajili
mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bony
(Daily Star). Share tetesi hizi na wapenda
soka wote. Tetesi nyingine kwenye magazeti
na mitandao ya Jumapili tukijaaliwa.
Cheers!etesi za soka katika magazeti ya ulaya
0 comments:
Post a Comment