Kuhusu Mchekeshaji Kansiime anavyotengeneza pesa Kenya.

Kansiime 1Kansiime Anne ni mchekeshaji kutoka Uganda ambae amesomea Sayansi ya saikolojia kwenye chuo kikuu cha Makerere Kampala Uganda ambako alianzia kuchekesha kama utani kusambaza video zake mitandaoni lakini kwa sasa anaingiza mamilioni baada ya kukubalika kwenye nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya....>>>

Kupenyeza kwake kwenye soko la uchekeshaji nchini Kenya ni jambo ambalo hata yeye anasema hakulitegemea kwa kiasi hicho lakini sasa amezidi kuwa maarufu kutokana na show yake ya TV iitwayo Don’t mess with Kansiime inayoonekana CitizenTV Kenya ambapo amezidi kupokelewa na Wakenya wengi wakiwemo ambao hubaki kwenye maeneo ya starehe mjini kumtazama kila Jumatano huku wakisubiria foleni ya magari ipungue ndio warudi nyumbani.
Anne anasema baada ya mda mrefu wa kukubalika na watazamaji wake youtube, kulimfanya siku moja apokee simu kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa CitizenTV Washira Waruru aliempa dili la kuanza kuonyesha show zake kwenye station hii.
Kansiime 2Mbali na CitizenTV Kenya, kansiime pia ameangukia dili ya mamilioni ya hela kama balozi wa bidhaa za kampuni ya bima na pia ameonekana kwenye tangazo la kibishara la Old mutual kuhusu kuwekeza akiba kwa ajili ya siku za usoni hasa bima ya watoto kwa ajili ya masomo ya shule ya upili, madili yote hayo yakiwa ya Kenya.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks