Watu 30 wauawa katika shambulizi, kenya

Mashambulizi katika eneo la Mpeketoni kenya

Wizara ya maswala ya ndani nchini Kenya inasema kuwa takriban watu thelathini wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makaazi ya pwani ya kenya karibu na mpaka wa Somali....>>>>

Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku tisa wengine wakiuawa kufuatia ufyatulianaji wa risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunty ya lamu karibu na mpaka wa Somali.
Inadaiwa kuwa watu walikuwa wakitizama mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoni ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa katika shambulizi jengine mwezi uliopita.

Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks