Carragher: ‘Torres hana jipya tena England’

katika kipindi cha miaka minne aliyoichezea Liverpool Torres alifunga magoli
Katika kipindi cha miaka minne aliyoichezea Liverpool Torres alifunga magoli 81 katika mechi 142
 Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza pamoja na klabu ya Liverpool Jamie Carragher, ameusifia uwamuzi wa Fernando Torres kuhama katika klabu ya Chelsea na akuelekea katika klabu ya Ac Milan kwa mkopo wa miaka miwili kwania ya kukiokoa kipaji chake kinachozidi kufifia kwa kasi ya ajabu....>>>>

‘Inauzunisha sana kumuona staa mwenye mkataba mnono katika klabu yake, akiwekwa benchi karibu katika kila mechi za mwisho wa wiki.”
‘Nadhani wakati wake katika ligi kuu ya England umekwisha, sidhani kama Torres anaweza akarudi katika kiwango cha juu akiwa na kikosi cha Chelsea kama alipokuwa akiichezea Liverpool kwa kipindi cha 2007/11.
‘Mimi binafsi nilikuwa na amini huwezi ukawa taja mastraika wanne wakali duniani halafu jina la Torres usilitaje,
Jamaa alikuwa na uwezo wakipeke wakulijua lango na kutupia magoli kambani, kwa ufupi alikuwa nitishio kwa mabeki wa timu pinzani.’
Hayo ni maneno Jamie Carragher katika mkutano na waandishi wa habari.
Katika kipindi cha miaka minne aliyoitumikia klabu ya Liverpool, Torres alifunga magoli 81 katika michezo 142 ambayo ni sawa na wastani wa goli 1.8 katika kila mchezo.
Bonasi au mtonyo aliokuwa akiupokea katika kila goli ililofunga akiwa na The Reds ni Tshs mil 740,
Na mchango wake katika kikosi ulionekana kuendana sawa na gharama za ada ya uhamisho wa pauni mil 24 (Tshs bil 60), kutoka Atletico Madrid msimu wa 2007/08.
klabu ya Chelsea ifanikiwa kumpata straika huyo katika msimu wa 2011/12 kwa ada iliyovunja rekodi za uhamisho katika kipindi hicho ya pauni mil 50 (Tsh bil 125),
Katika kipindi cha miaka mitatu akiwa na The blues, Torres alifunga magoli
Katika kipindi cha miaka mitatu akiwa na The blues, Torres alifunga magoli 45 katika mechi 172
lakini kinyume na matarajio ya wengi Torres hakuweza kufikia hata robo ya uwezo wake uwanjani wakutupia na kutoa ‘assist’ za magoli kama alivyokuwa akifanya akiwa na
kikosi chake cha The Reds licha ya mkwanja mrefu aliokuwa akiungiza katika akaunti yake.
Katika muda wote aliokuwa na kikosi cha The Blues, Torres alifunga magoli 45 katika mechi 172 sawa na wastani wa magoli 3.8 kwa kila mechi,
pia alikuwa akipokea bonasi ya pauni mil 1.1 (Tshs bil 2.75) katika kila goli analofunga, kiwango kisicho lingana na mchango wake katika timu.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks