Hofu ya Ebola yatibua mipango yakina Yaya Toure

kikosi cha Ivory Coast
kikosi cha Ivory Coast kitakocho cheza na Sierra Leone
Shirikisho la soka la Ivory Coast limesema kuwa huenda likasusia mechi ya kufuzu katika michuano ya mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao Sierra Leone wakihofia maambukizi ya ugonjwa wa Ebola...>>

Mchezo huo ambao umepangwa kuchezwa mjini Abidjan tarehe 6 Septemba umeibua taharuki miongoni mwa maafisa wa Afya na pia serikali kuu imetishia kupiga marufuku kufanyika kwa mchezo huo.
Hofu hiyo inatokana na kuenea kwa homa ya Ebola katika mataifa matano kanda ya Afrika Magharibi ikiwemo Sierra Leone.
Tayari Sierra Leone imetaja kikosi cha wachezaji wanaocheza njee ya Sierra Leone ilikuepusha hatari ya kueneza Ebola Ivory Coast .
Vilevile Sierra Leone imeagiza maafisa wote wa ukufunzi kufanyiwa uchunguzi wa kutosha kabla ya kuingia Ivory Coast .
Hata hivyo Shirikisho la soka barani Afrika limekataa katakata kubadilisha sehemu itakapoandaliwa mechi za kufuzu licha ya hatari ya maambukizi .
Hadi kufikia sasa haijulikani iwapo CAF itaichukulia hatua zaidi Ivory Coast iwapo itasusia kucheza na Sierra Leone au itaruhusiwa kuendelea na mechi za kufuzu
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks