Shirika la Afya Duniani (WHO) limeiweka Kenya katika “hatari ya juu” kama taifa litakalosambaa virusi vinavyoua vya Ebola.
Kenya iko hatarini kwa sababu ni moja ya kitovu kikubwa cha usafiri, ndege nyingi hutoka Afrika Magharibi, alisema afisa wa Shirika la Afya...>>>>
Hili ni moja ya onyo makini lililotolewa na WHO kwamba Ebola inaweza kusambaa Afrika Mashariki.
Wataalamu wa afya wanapambana kuzuia mlipuko Afrika Magharibi, ambao umeshaua zaidi ya watu 1,000.
Canada imesema itatoa msaada wa dozi 1,000 wa majaribio ya kinga dhidi ya Ebola ili kusaidia mapambano dhidi ya mlipuko huo.
0 comments:
Post a Comment