Arsenal inamtolea macho nyota wa Borussia Dortmund Marco Reus kuchukua nafasi ya Theo Walcott.
Winga wa Uingereza alianza kumuudhi Arsene Wenger kwa kudai mazungumzo ya mkataba mpya bado hayajaanza, pamoja na kwamba kocha huyo wa Washika Bunduki amerudia kuzungumza kinyume.
Wenger alithibitisha lengo la klabu hiyo kumpa mkataba mpya Walcott tangu Februari na alipoulizwa kuwa mazungumzo yalianza Machi 13, kocha huyo alijibu: “Mazungumzo ya kwanza yalishafanyika na tutaona yatakavyoendelea.”
Hata hivyo, Walcott, ambaye kwa sasa analipwa pauni 90,000 kwa wiki, aliandika kwenye Twitter kumchanganya kocha wake.
Nyota huyo 26, anataka mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki kusaini mkataba mpya kwenye Uwanja wa Emirates.
Akiwa hana uhakika kucheza kikosi cha kwanza, pia uongozi wa Arsenal unaonekana kukataa kufikia mahitaji ya Walcott.
Vilevile, Walcott anaonekana kuchangikiwa kwa kukosa mechi baada ya kurudi kutoka kwenye majeraha ya goti ya muda mrefu.




0 comments:
Post a Comment