Mkalia benchi wa Manchester United Radamel Falcao alituma ujumbe kwa Louis van Gaal kwa kufunga magoli mawili wakati Colombia ikicheza mechi ya kirafiki na Bahrain Alhamisi usiku.
Falcao alifunga magoli mawili kwa Colombia, goli la pili na la tatu katika ushindi wa kishindo wa 6-0 dhidi ya timu inayoshika nafasi 103 duniani kwenye Uwanja wa Taifa wa Bahrain.
Mbali na hivyo, Falcao alikuwa msaada kwa mshabuliaji mwenzake Carlos Bacca akifunga dakika ya 14 baada ya Juan Cuadrado wa Chelsea kugongesha mwamba.



0 comments:
Post a Comment