Rubani Andreas Lubitz huenda amekuwa akisumbuliwa na matatizo binafsi wakati wa ajali ya ndege ya Germanwings, ilidaiwa usiku uliopita.
Taarifa kutoka Ujerumani zilidai kuwa kijana huyo 28 alikuwa akijaribu kukubaliana na hali baada mahusiano yake kuvunjika wakati alipoigongesha makusudi ndege ya A320 kwenye mlima, na kuua abiria 149.
Hali hiyo ilijulikana masaa kadhaa baada ya polisi kuchunguza ajali hiyo iliyotangazwa na kudai wamepata uchunguzi makini uliochukua saa nne kwa kuchunguza nyumba ya Lubitz, aliyokuwa akiishi na mpenzi wake.
Maafisa hao walikataa kuvujisha taarifa hizo muhimu bali walilisitiza haikuwa taarifa ya kujiua kwa makusudi

Mabaki ya ndege: Timu zikifanya uchunguzi kupata mali na miili ya watu waliokuwepo kwenye ndege hiyo
Jana, bosi wa Lubitz alikubali kuwa kama angelijua hilo asingemruhusu kurusha ndege.
Pia Iligunduliwa kuwa mpenda mazoezi huyo alikuwa na msongo wa mawazo ambao ulimuandama hadi kwenye kazi yake.
Lakini, cha kushangaza, alipita vipimo yote ya akili na kuruhusiwa kurusha ndege.



0 comments:
Post a Comment