Polisi nchini Afrika Kusini wamesema wanachunguza chanzo ajali ya barabarani iliyomuua waziri wa utumishi wa umma na utawala Collins Chabane.
Chabane, dereva na walinzi wake walipoteza maisha papo kwa hapo katika ajali hiyo iliotokea katika jimbo la kaskazini la Limpopo mapema leo.
Dereva wa lori lililosababisha ajali hiyo hakujeruhiwa na analaumiwa kwa kutofuata sheria za barabara kuu.
Msemaji wa polisi kwenye jimbo la Limpopo Kanali Ronel Otto amesema dereva wa lori hilo hajakamatwa kutokana na kwamba hawajafanya uchunguzi kamili, ameongeza kuwa polisi watawasilisha kesi mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment