Hii ndo Barua ya Zitto Kabwe ya kung’atuka bungeni


Zitto Kabwe
Zitto Kabwe
Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zubeir Kabwe ameliandikia barua bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza kung’atuka katika bunge hilo.
Zitto ambaye alikuwa mbunge kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia alifanya maamuzi hayo baada ya kuvuliwa uanachama wake mapema mwezi Machi.
Barua ya Zitto Kabwe aliyoiandikia bunge kutangaza kuachia ubunge
Barua ya Zitto Kabwe aliyoiandikia bunge kutangaza kuachia ubunge
Mbunge huyo machachari amemaliza sintofahamu za wananchi pamoja na bunge hasa baada ya Spika wa Bunge kusema kuwa hatambui kuvuliwa kwa ubunge wake wakati walipoanza vikao vya bunge Machi 17, 2015.
Kwa sasa msomi huyo wa uchumi ambaye alisema hagombei tena ubunge anatarajiwa kuhamia chama cha ACT (Alliance for Change and Transparency) kinachotarajiwa kuzinduliwa rasmi Machi 29, 2015.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks