Kuhusu sheria mpya kutoka india inayohusiana na mitandao ya kijamii

face
FacebookTwitter na Instagram imekuwa sehemu ya mitandao maarufu kwa watu kushare taarifa mbalimbali, lakini kutokana na mitandao hii kukua kwa kasi mara nyingi kumekuwa na mvutano juu ya sheria ambazo zinawekwa ili kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
India walipitisha sheria ambayo tayari kuna watu wako kifungoni kutokana na kukiuka sheria hiyo, lakini leo kuna taarifa tofauti inayohusu ishu ya Mahakama Kuu India kufuta kipengele cha sheria kilichokuwa kikiamrisha mtu yoyote akiandika ujumbe wa kichochezi kwenye mtandao ashitakiwe.
Kulingana na kipengele hicho watu walioikashifu Serikali na idara zake India walikuwa wakikamatwa na kufungwa kifungo mpaka cha miaka mitatu.
Mwaka 2012 wasichana wawili walikamatwa Mumbai kwa kutoa maoni yao kufuatia mauaji ya mwanasiasa maarufu Bal Thackeray, mwingine alikamatwa kwa ishu ya kukashifu Serikali, lakini yupo aliyefungwa kutokana na ku’like” ujumbe huo.
Kumekuwa na idadi kubwa ya wanaharakati waliokamatwa kutokana na sheria hiyo ambayo mara zote imekuwa ikipingwa kwamba ni ya kikatili.
Millard ayo
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks