Leo ni Jumamosi tarehe 16 Mfunguo Nane Jamad al-Awwal 1436 Hijria sawa na tarehe 7 Machi mwaka 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 741 iliyopita, alifariki dunia mwanafalsafa wa Kitaliano Thomas Aquinas. Alizaliwa mwaka 1225 katika mji wa Napoli na kupata elimu ya dini katika mji huo hadi chuo kikuu. Mwanafikra huyo alibuni falsafa makhususi na kutambua kwamba saada na ufanisi mkubwa zaidi wa mwanadamu ni kupiga hatua za kuelekea kwenye ukamilifu wa kiroho na kwa Mwenyezi Mungu. Aquinas kama alivyokuwa Aristotle, aliamini kuwa ndani ya nafsi ya kila mwanadamu kuna nguvu inayoweza kumfikisha kwenye ukamilifu wa kiroho. Vilevile aliamini kwamba teolojia haipingani na sayansi kwani kila moja kati ya viwili hivyo inataka kujua hakika na kweli. Itikadi za Aquinas na misimamo yake ya kutumia akili na mantiki ambayo ilikuwa ikipingwa vikali na kanisa katika karne za kati, ilisaidia sana kueneza elimu.
***
Katika siku kama ya leo miaka 64
iliyopita, aliuawa Ali Razmara, Waziri Mkuu wa Iran aliyekuwa kibaraka
wa Uingereza. Razmara aliyekuwa jenerali wa jeshi katika utawala wa
kifalme aliuawa na mwanamapinduzi wa Kiislamu aliyejulikana kwa jina la
Khalil Tahmasbi. Usaliti na uovu wa wazi wa Ali Razmara katika siasa za
kuiongoza nchi, ulizusha upinzani mkubwa wa wananchi dhidi ya Waziri
Mkuu huyo na kutayarisha mazingira ya kuangamizwa kwake.
***
Katika siku kama ya leo miaka 776 Ibn
Abdus Salaam fakihi, kadhi na khatibu wa Kiislamu aliaga dunia mjini
Cairo Misri. Alijifunza fiq'hi na hadithi na kwa muda mfupi akaibuka na
kuwa mmoja wa maulama mahiri wa zama zake. Ibn Abdus Salaam alipitisha
kipindi cha umri wake katika zama za mivutano na mapigano baina ya
Waayubi kwa upande mmoja na Waayubi na jeshi la msalaba.
***
Na katika siku kama ya leo miaka 250
iliyopita alizaliwa Nicephore Niepce mwanakemia wa Kifaransa na mmoja wa
waasisi wa fani ya upigaji picha. Niepce alikuwa mtu wa kwanza
aliyefanikiwa kupiga picha ya kwanza duniani. Baada ya hapo, Nicephore
alitengeneza kamera ya kupiga picha kwa kushirikiana na marafiki zake.
Mwanakemia huyo wa Ufaransa aliaga dunia mwaka 1833.
0 comments:
Post a Comment